Tuesday, 4 October 2016

DONALD TRUMP ATAKA KUFANYA MKUTANO NA WAISLAMU WA MAREKANI

Mgombea wa urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican Donald Trump ambaye ni maarufu kwa kauli za ubaguzi dhidi ya waislamu ameomba kufanya mkutano pamoja na waislamu .
Hata hivyo katibu mkuu wa shirika la waislamu wa Marekani (USCMO) ,Osama Jamal alisema kuwa ombi la Trump halikukubaliwa kipindi cha sherehe za Eid Ul Adha .

Wakati wa sherehe za Eid Ul Adha Trump alifanya kampeni zake za uchaguzi katika bustani la Toyota Park mjini Chicago ambapo takriban 25,000 walihudhuria .

Katika Kampeni hizo Donald Trump alidokezea mpango wake wa kukutana na jumuiya ya waislamu ya USCMO na kuongea na wao masuala kadhaa.

Hata hivyo Osama Jamal alibainisha  kuwa jamii ya waislamu haina tatizo lolote na Trump na kuwa watakubali kufanya mkutano na mgombea huyo wa urais .

Wakati huo huo Osama alisema kuwa jumuiya ya waislamu ipo wazi kufanya mazungumzo na wagombea wote wa urais wa Marekani kwa sababu uchaguzi mkuu ni muhimu kwa jamii ya waislamu nchini humo.

Jamal alitoa wito kwa waislamu wote nchini humo kujitokeza huku takwimu zikionyeshakuwa nchini Marekani waislamu takriban milioni moja wamejiandikisha kama wapigaji kura .