KATIKA mkutano wa kuwasilisha utekelezaji wa haki za binadamu uliofanyika geneva, Uswisi 22 september 2016, Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu mkuu wa Wizara ya katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome wamekataa mapendekezo ya Marekani ya kuunda sheria ya haki za binadamu inayokubali ushoga na ndoa za jinsia moja.
Akizungumza jana katika kipindi cha mada moto kinachorushwa na televisheni ya Channel 10, Waziri wa katiba na sheria mh. Dkt. Harrison Mwakyembe alisema walipewa mapendekezo 202 katika ya hayo wamekubali mapendekezo 130 na kuyakataa mengine.
Aidha amesisitiza kwamba kamwe serikali haitakubali kutunga sheria za kuruhusu ushoga, ndoa za jinsia moja kwa kuwa ni kinyume na taratibu za nchi, tamaduni na ustaarabu wa watanzania.
Akizungumza kwa hisia kali aliongeza kusema kwamba utamaduni huo ni upuuzi na wala si sehemu ya haki za binadamu kama wanavyodai mataifa ya ulaya.
Pia amezionya NGO zinazohusiana na masuala ya afya kutojihusisha katika kusaidia mambo ya ushoga na yoyote itakayobainika itachukuliwa hatua za kisheria.
Kwa muda mrefu mataifa makubwa yamekuwa yakishinikiza mataifa madogo hususa yaliyo katika bara la Afrika kuruhusu na kutambua ushoga na ndoa za jinsia moja
