Nyota wa Ujerumani mwenye asili ya Albania ambaye anachezea klabu ya Arsenal Shkodran Mustafi, ametoa maelezo kuhusu imani yake ya dini ya Kiislamu.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 24 alifanya mahojiano na gazeti la The Sun na kubainisha umuhimu wa kuwa na imani ya dini ya Kiislamu.
Akifahamisha nia yake ya kutaka kutekeleza ibada ya Hijjah, Mustafi alisema, ‘‘Uislamu ni muhimu kwangu kuliko kila kitu.’’
Mustafi pia aliarifu ugumu anaopitia wakati mwingine katika jitihada za utekelezaji wa baadhi ya ibada za Kiislamu hasa katika mwezi mtukufu wa Ramadhan kutokana na uchezaji.
Mustafi alisema, ‘‘Najivunia na kufurahia kuwa Muislamu. Siku moja nitatekeleza ibada ya Hijjah ambayo tunatakiwa kutimiza angalau mara moja maishani na hilo ndilo lengo langu kuu.’’
