Saturday, 15 October 2016

MSIKITI WA AL AQSA WAIDHINISHWA KUTOHUSIANA NA DINI YA UYAHUDI

UNESCO imekubali muswada unaopinga dini ya Kiyahudi kuhusika na msikiti wa Al-Aqsa mjini Jerusalem.

Muswada huo uliowasilishwa kwa kamati ya UNESCO ya kushughulikia masuala ya nje ulikubaliwa baada ya kupitishwa kwa kura 24 dhidi ya 6.
Wanachama wawili hawakushiriki kwenye mchakato wa upigaji kura.

Katika muswada huo, ilibainishwa kwamba msikiti wa Al-Aqsa ulioko mjini Jerusalem unahusiana na dini ya Kiislamu na Kikristo.

Dini ya Kiyahudi inayotokea nchini Israel ilipingwa kuhusiana na msikiti wa Al-Aqsa.

Miongoni mwa nchi zilizopigia kura muswada huo ni Ufaransa, Marekani, Ujerumani na Uingereza.

Baraza kuu la UNESCO linalojumuisha wanachama 58 litapiga tena kura siku ya Jumatatu ili kuidhinisha muswada huo.

kwa muda mrefu wayahudi wamekuwa wakiushikiria msikiti huo kwa mabavu kwa kuunasibisha na dini yao.