Msikiti wa Fatih uliojengwa na muungano wa Kiislamu wa Kituruki DİTİB mjini Dresden nchini Ujerumani umeripotiwa kushambuliwa kwa vilipuzi.
Mashambulizi hayo yameripotiwa kutekelezwa hapo jana usiku mwendo wa saa 2.00 Usiku.
Kamera za siri zimeweza kurekodi tukio hilo mwanzo hadi mwisho.
Kulingana na rekodi ya kamera, mtu mmoja alionekana akisimama mbele ya eneo la imamu na kutega chupa za gesi ambapo baadaye mlipuko mkubwa ulitokea.
Moto mkubwa ulitokea baada ya mlipuko na majirani waliokuwa karibu wakafanikiwa kuukabili na kuuzima.
Balozi wa Uturuki nchini Ujerumani Ahmet Başar Şen aliwasili katika eneo la tukio ambalo lipo umbali wa kilomita 200 kutoka mji mkuu wa Berlin na kuarifiwa kutokuwepo kwa vifo wala majeruhi.
Başar Şen alitoa wito kwa viongozi wa Ujerumani kuanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo.
Mashuhuda wa tukio hilo wametoa maelezo na kufahamisha kwamba mshambuliaji alitoroka kwa pikipiki kabla ya polisi kupewa taarifa.
Siku 3 zilizopita, msikiti wa Mimar Sinan unaosimamiwa na DİTİB mjini Bebra mkoani Hessen pia uliwahi kushambuliwa kwa vilipuzi vya chupa na kusababishiwa uharibifu wa hasara ya Euro elfu 10.
