Sunday, 4 September 2016

RAIS MUSEVENI, OMAR BASHIR WASAFIRISHA WAGANDA 100 KWENDA KUHIJI MAKKA MWAKA 2016

Rais wa Uganda Yoweri museveni akishirikiana na Rais wa Sudan Omar Bashir wamewasafirisha waislamu wapatao 100 kwa ajili ya kwenda nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kutekeleza ibada Tukufu ya Hijja.
Akisalimiana na Ahmed Karegga Musaazi
Mahujajaji hao waliondoka jana baada ya kuagwa na Rais Museveni katika Ikulu ya Uganda iliyopo Entebbe. Kundi la kwanza liliondoka tangu tarehe 26 ya mwezi August 2016.
Rais museveni akipungia bendera ya Uganda kuashiria kuanza safari
Waganda 800 wanatarajiwa kufanya Hijja mwaka huu.