Sunday, 28 August 2016

ASKARI WA KIKE WARUHUSIWA KUVAA HIJABU KATIKA JESHI LA POLISI UTURUKI

Wanawake katika jeshi la Polisi nchini Uturuki wamepewa ruhusa  ya kuvaa hijabu wanapokuwa kazini kwa masharti ya kuheshimu sheria kama inavyofahamisha katika sheria za mavazi katika jeshi la Polisi.
Taarifa hiyo ilitolewa katika jarida la taifa Jumamosi jana linalojulikana kama Hurriyet.

Marekebisho katika kifungu nambari 5 katika sheria hiyo kwa polisi kinaruhusu wanawake kuvaa hijab juu ya kofia zao kwa sharti kuwa hijabu hizo ziwe za rangi ya sare na zisiwe na michoro.

Marufuku ya kuvaa hijabu katika ofisi za umma ilitolewa mwaka 2013 ambapo rais Erdogan alikuwa ni waziri mkuu wa Uturuki.