Tuesday, 6 September 2016

MARUFUKU YA HIJABU KATIKA HOSPITALI KWA WAUGUZI YAONDOLEWA NCHINI NIGERIA

Utawala wa hospitali moja ya taifa iliyoko mjini Abeokuta kusini magharibi mwa Nigeria umetangaza kufutilia mbali marufuku ya hijabu yaliyokuwa wamewekewa wauguzi.
Afisa mmoja mkuu wa hospitali hiyo alitoa maelezo na kutangaza kuruhusu wanawake wa Kiislamu wanaofanya kazi kama wauguzi kujitanda hijabu hadi mabegani.

Afisa huyo aliarifu kutia saini kanuni hiyo mpya na kufutilia mbali marufuku yaliyokuwa yamewekwa siku ya Jumatano dhidi ya wauguzi wa Kiislamu.

Chama cha kutetea haki za Waislamu cha MURIC nchini humo kilitoa malalamiko kuhusiana na suala la marufuku baada ya kupokea ripoti ya kuzuiwa kwa wauguzi wenye hijab kuingia hospitalini siku ya Jumatano.

Chama hicho pia kilikumbushia kutokuwepo kwa kanuni kama hiyo ya kuzuia wauguzi kufanya kazi katika hospitali za taifa.