Thursday, 8 September 2016

BAKWATA YATANGAZA SIKUKUU YA EID ADH-HA NI SIKU YA JUMATATU

Baraza kuu la waislamu Tanzania (Bakwata) limetangaza
rasmi kwamba sikukuu ya Eid adh'ha maarufu kama Eid el hajj itakuwa siku ya jumatatu tarehe 12 Septemba mwaka huu.
Katika taarifa yake iliyotoa kwa vyombo vya habari imesema kitaifa swala ya Eid el Hajj itafanyika katika viwanja vya Bakwata makao makuu Kinondoni jiji dar es salaam.

Sikukuu ya Eid el hajj hufanyika kila mwaka baada ya waislamu walioko Makka kumaliza ibada yao tukufu ya kufanya Hijja.

Aidha, imesuniwa kufunga kwa waislamu masiku kumi ya mwezi wa dhulhijja na yule ambaye atashindwa kufanya hivyo basi ajitahidi afunge ndani ya mwezi Tisa ya Dhulhijja.

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir anawatakia Waisamu wote na wananchi kwa ujumla Eid Adh-ha njema