Friday, 26 August 2016

MJADALA WA KUTAMBUA UISLAMU KAMA DINI RASMI WAPENDEKEZWA USWIZI

Mwenyekiti wa chama cha kijamii na demokrasia (Social Democratic Party) cha Uswisi Christian Levrat, amependekeza Uislamu kutambulishwa kama dini rasmi nchini.
Christian Levrat
Levrat alitoa pendekezo hilo kwenye maelezo yake yaliyochapishwa na gazeti la Sonntags Zeitung na kuarifu kwamba suala la kutambulika kwa Uislamu kuwa dini rasmi kikatiba linapaswa kujadiliwa.

Katika pendekezo lake, Levrat alisema, ‘‘Endapo Uislamu utatambulishwa kama rasmi, viongozi na walimu wa kidini watapokewa vizuri zaidi na jamii nchini Uswisi.’’

Maelezo ya Levrat pia yalipewa nafasi kubwa kwenye taarifa za gazeti la 20 Minuten.

Katika taarifa hizo, kuliandaliwa hoja na maoni kuhusiana na swali la ‘‘Je, Uislamu unapaswa kutambulishwa kama dini rasmi nchini Uswisi?’’