Saturday, 27 August 2016

MISIKITI, SHULE ZA KIISLAMU, HIJABU, QURANI KUPIGWA MARUFUKU UHOLANZI NA CHAMA CHA SIASA

Chama cha siasa cha Freedom Party (PVV) kinachoongozwa na Geert Wilders kimeapa kwamba endapo kitaongoza katika uchaguzi ujao mwakani kitapiga marufuku Misikiti na Qurani
nchi Uholanzi kama ilani yao ya uchaguzi inavyosema.
Geert Wilders
"Misikiti yote, shule za kiislamu na Qurani vitapigwa marufuku", ilisema taarifa iliyotolewa na chama
hicho kuelekea uchauzi wa wabunge Machi 2017 katika ukurasa wake wa Twitter Alhamisi ya jana.

Taarifa hiyo ambayo ipo katika Ilani yake ya Uchaguzi ujao, ilisema itachukua hatua mbalimbali ikiwemo kufunga mipaka, kufunga vituo vya wakimbizi, kuzuia wahamiaji kutoka nchi za kiislamu na kuzuia wanawake wa kiislamu kuvaa Hijabu katika maeneo ya Umma.

Chama hicho kina viti 12 kati ya 150 ambapo kina imani katika uchaguzi ujao kushinda viti vingi zaidi. 

Geert Wilders ambaye ndiye anayekiongoza chama hicho anatajwa kama mtu anayeongoza kwa chuki dhidi ya uislamu duniani. 

Geert Wilders amekuwa akienda popote duniani ili kutoa mchango wake katika harakati za kuukandamiza Uislamu.