Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mmoja miongoni mwa viongozi wa dili ya uislam nchini Burundi Haruna Nkunduwiga ni kwamba idadi ya mahujaji mwaka 2016 imepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na hali ya usalama na kisiasa isioridhisha nchini.
Idadi ya mahujaji watakao shiriki ibada ya hija ya mwaka 2016 inaonekana haitozidi mahujaji 60.
Haruna Nkunduwiga amefahamisha kuwa mwaka 2015 wahujaji 150 ndio waliodiriki ibada hiyo ambayo ni moja ya nguzo 5 za uislamu.
Safari za hija mwaka 2016 zimegawika makundi mawili ambapo kundi la kwanza litaanza safari yake ifikapo Agosti 30 huku kundi la pili Septemba mosi.
