Watu hao wamepigwa risasi kichwani kwenye eneo la Ozone Park, hatua chache kutoka Al-Furqan Jame Masjid, kwa mujibu wa mashuhuda na mamlaka za serikali.
Imam Alala Uddin Akongi ni kiongozi wa kidini aliyeheshimika sana tangu alipowasili katika mji huo akitokea Bangladesh miaka miwili iliyopita.
Msaidizi wake, Thara Uddin mwenye umri wa miaka 64, alijeruhiwa vibaya sana na baadaye kufariki dunia baada ya kufikishwa hospitali.
Wote wawili walikuwa wamevaa mavazi ya Kiislamu waliposhambuliwa, na waumini wa msikiti huo wamelaani shambulizi hilo na kulitaja kuwa ni uhalifu wa chuki.
![]() |
| imamu aliyeuawa |
“Marekani haikua hivyo,” alisema mkazi mmoja wa eneo hilo, Khairul Islam, mwenye umri wa miaka 33. “Tunamlaumu Donald Trump kwa hili ... Trump na maigizo yake ndio ametengeneza Islamophobia (chuki dhidi ya Uislamu).”
Polisi wanasema kuwa waliitikia ripoti za tukio hilo saa 8:00 mchana kwa majira ya New York.
![]() |
| Thara Uddin, Imamu msaidizi |
Kampeni ya mgombea wa Urais wa Marekani kupitia chama cha Republican imekuwa ikitawaliwa na kauli tata dhidi ya jamii za watu wachache wanaoishi nchini humo.
![]() |
| Waislamu wakiandamana kupinga mauaji hayo |
Aidha, amekuwa akisema kuwa ataweka hifadhi data maalumu ya kuwafuatilia Waislamu wote na kwamba Marekani haitakuwa na chaguo jingine bali kuifunga misikiti yote.
| Wakiomba Dua |



