Wizara ya Mazingira ya nchini Ugiriki imewasilisha Bungeni muswada utakao tatua suala la ujenzi wa Msikiti
katika mji wa Athens.
Muswada huo wa dharura utapigiwa kura Alhamis ya wiki hii na wabunge wa bunge hilo.
Ripoti iliyowasilishwa bungeni inasema kutokuwepo kwa msikiti katika mji huo kunaipa picha mbaya nchi hiyo katika nyanja za kimataifa.
Mpango wa ujenzi wa msikiti katika mji huo umekuwa unakabiliwa na ucheleweshwaji mbalimbali hususani Kanisa lenye nguvu la Orthodox ambalo kwa muda mrefu limepinga ujenzi wa msikiti katika mji huo.
Athens imekosolewa na makundi ya haki za binadamu kama vile Amnesty International kwa kuwa mji mkuu wa Umoja wa Ulaya bila msikiti.
Athens ni moja ya miji mikuu michache ya Ulaya ambayo haina msikiti.
Kwa mara ya mwisho kuwepo msikiti katika mji huo ni pale ulipoanguka utawala Uthmani bin Affan.
Waislamu wanakadiriwa kuwa 300,000 katika mji wa Athens na wamekuwa wakisali katika maghala na sehemu zisizo rasmi kwa ajili ya kutimiza ibada za swala.
