Monday, 1 August 2016

MKUTANO WA WASOMA MAULID YA MTUMEﷺ TANZANIA WAMALIZIKA MKOANI KAGERA

Mkutano wa shirikisho la wasoma Maulidi ya Mtume Muhammadﷺ Tanzania uliofanyika jana eneo la kibuye, Bukoba Mjini Mkoani Kagera nchini Tanzania umefungwa rasmi na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir.
Mkutano huo uliofanyika kwa siku tatu, Mufti ambaye alikuwa mgeni rasmi wa Mkutano huo, alizindua rasmi shirikisho hilo la wasoma Maulid Tanzania (shiwamat).

Aidha katika mkutano huo yamepitishwa maadhimio kadhaa ikiwemo Shirikisho lisiwe na uongozi wa kudumu bali uongozi wake uwe wa mzunguko wa kila mkoa kuongoza kwa mwaka mmoja na kupitisha uongozi kwa mkoa mwingine.
Mkutano huo umechagua kiongozi mpya ambaye atakuwa ni Sheikh Abdurafiu bin Alhaji Jaafari wa Mkoa wa Kagera kuchukua uongozi uliokuwa kwa Sheikh wa Mkoa wa Mwanza.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe kutoka taasisi za kiislamu, misikiti na Masheikh mikoa mbalimbali ya Tanzania pamoja na kutoka nchi za Kenya Uganda Burundi na Congo.

Mkutano huo ambao ni wa nne kuandaliwa, wa kwanza ulifanyika nzega mkoani Tabora, wa pili sengerema mkoani mwanza na wa tatu Nyamagana mkoani mwanza.
Pia Mkutano huo ulimuomba Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir kuwa Mlezi wa shirikisho hilo na alikubali.

Picha na maelezo kwa ihsani ya 
Sheikh Hassan Kabeke