Tuesday, 19 July 2016

WANAWAKE WAISLAMU 10,000 WAJITOKEZA KUTAKA KUOLEWA NIGERIA

Zaidi ya wanawake waislamu 10,000 wameomba watafutiwe waume watakaowaoa.

Wanawake hao wameomba shirika la kiislamu la Hizba linalohudumu katika jimbo la Kano lililoko kaskazini mwa Nigeria kuwaunganisha na kugharamia ndoa ya halaiki.
Kamati maalum ya Hizba ndiyo iliyopewa jukumu hilo la kuwaozesha maelfu ya wanawake waislamu.

Madhumuni ya kamati hiyo ya Hizba ni kupunguza idadi ya wanawake waislamu ambao hawajaolewa.

Hizba huwakutanisha wanawake na wanaume waislamu kwa lengo la kuwaoza kama watakubaliana kwa misingi ya dini ya kiislamu. Hakuna tarehe maalum iliyotengwa

Takriban wanandoa 5,000 wamefunga pingu za maisha tangu mradi huo uanzishwe mwka wa 2012.