Wednesday, 20 July 2016

MUFTI WA TANZANIA, KADHI MKUU WAONGOZA MAMIA YA WAUMINI KUMZIKA SHEIKH KHAMIS SAID KHALFAN

Mamia ya waumini wa kiislamu wamejitokeza kumzika Sheikh Khamis Said Khalfan katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Mufti wa Tanzania katikati akiwana na Kadhi Mkuu kulia kwake Sheikh
Abdallah Mnyasi na kushoto ni Sheikh Alhad Omar
Shughuli za mazishi pamoja na visomo vilifanyika katika msikiti wa Shadhily ulioko Mtaa wa Twiga, Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto Sheikh Suleiman Kilemile, Sheikh Hassan Chizenga na Sheikh Hamid Jongo.
Masheikh wengi walihudhuria wakiongozwa na Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir na Kadhi Mkuu wa Tanzania Sheikh Abdallah Mnyasi.
Masheikh
Wengine waliohudhuria ni Sheikh Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa, Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Hamid Jongo, Sheikh Alhad Omari Alhad, Sheikh Hassan Chizenga, Sheikh Walid alhad imamu wa Msikiti wa Kichangani, Sheikh Abbas Ramadhani, Sheikh Ali na Sheikh Suleiman Amran Kilemile
Wengine ni Mkurugenzi wa zamani wa NSSF Dr. Ramadhani Dau, Mwenyekiti wa CCM mkoa Dar es Salaam Ramadhani Madabida na wengine wengi miongoni mwa Masheikh na watu mashuhuri wa ngazi tofauti.
Kutoka kushoto Ramadhani Madabida, Sheikh Suleiman Kilemile na Sheikh Hassan Chizenga.
Waumini Msikitini Shadhily
Waumini Msikitini Shadhily
Mwenyezi Mungu amsamehe makosa yake na alifanye kaburi lake kuwa miongoni mwa Mabustani ya peponi. 

Picha zote kwa ihsani ya 
Ustaadh Kassim Rashid