Tuesday, 19 July 2016

SHEIKH KHAMIS SAID KHALFAN KUZIKWA LEO ALASIRI, DAR ES SALAAM

Sheikh Khamis Said Khalfan anatarajiwa kuzikwa leo katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Shughuli za visomo zitaanza kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa sita za mchana nyumbani kwake Temeke Mtoni.
Baada ya hapo shughuli zitahamia katika Msikiti wa Shadhily ulioko Kariakoo mtaa wa twiga jijini dar es salaam pamoja na kusaliwa msikitini hapo.

Mwili utazikwa alasiri katika makaburi ya kisutu.
Sheikh Said alifariki jana katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili.

Taarifa ya kifo na historia yake kwa ufupi bonyeza hapo chini:
BREAKING NEWS: SHEIKH KHAMIS SAID AFARIKI LEO DUNIA LEO