Friday, 8 July 2016

VAZI LA BURQA LAPIGWA MARUFUKU NCHINI USWISI

Kanuni ya marufuku ya vazi la Burqa imeanza kufanya kazi rasmi katika eneo la Ticino lililoko upande wa kusini mwa Uswisi.

Kanuni hiyo imetangazwa kupiga marufuku wanawake kujifunika nyuso zao kwa vazi la burqa hasa katika maeneo ya wazi ya umma.

Watu watakaokiuka kanuni hiyo watatozwa faini ya fedha kuanzia Franc 100 hadi 10,000.
Kulingana na vyanzo vya habari vya Uswisi, mwanamke mmoja aliyekuwa amevalia vazi la burqa alikamatwa na polisi na kufikishwa kituoni mjini Locarno muda mfupi baada ya marufuku hayo kutangazwa.

Mwanamke huyo alitozwa faini ya fedha Franc 230 kwa ukiukaji wa sheria.

Ubalozi wa Saudi Arabia ulioko mjini Bern umetoa tahadhari kwa raia wake kuzingatia sheria hiyo watakapozuru Uswisi kuanzia tarehe 1 Julai.