Friday, 8 July 2016

MAHUJAJI WOTE WA MWAKA 2016 KUVAA VIKUKU VYA HI-TECH

Saudi Arabia imeamua kuunda vikuku vya elektroniki vitakavyovaliwa na mahujaji wa mwaka 2016 na miaka mingine ijayo kwa lengo la kiusalama .

Bangili hizo zimetengenezwa kwa namna ya kuwa zitaweza kuwa na taarifa ya binafsi ya mtu itakayosaidia mamlaka ya kutoa huduma za dharura wakati wa maafa .
Aidha vikuku hivyo pia vina uwezo wa kuzuia maji kuingia na vilevile kuunganishwa na GPS.

Mbali na hilo ni kuwa vitaweza kuwatambulisha mahujaji nyakati za sala na kuwa mwongozo kwa wale wasiojua lugha ya kiarabu.

Utengezaji wa bangili hizo umefanywa baada ya maafa mabaya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya kufanya hajj kufanyika mwaka jana .