Thursday, 14 July 2016

UNESCO YAKANUSHA KUTOA CHETI CHA DINI YA AMANI DUNIANI

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limesema kuwa habari iliyoenezwa kuwa imeitaja dini tukufu ya Kiislamu kuwa ndiyo dini ya amani zaidi duniani ni taarifa ya uongo.

UNESCO imesema taarifa hiyo iliyochapishwa na tovuti ijulikanayo kama juntakreporter iliyodai kuwa imetoa cheti ikisema, "Uislamu ni dini ya Amani duniani" si ya kweli na ni uongo mtupu.

UNESCO imesema haijawahi kutoa taarifa kama hiyo na kwamba cheti kilichochapishwa katika tovuti hiyo ni bandia. UNESCO imesema tovuti hiyo kwa kawaida huchapisha habari za vichekesho.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, "UNESCO haijawahi kuwa na uhusiano wowote na 'Taasisi ya Kimataifa kwa Ajili ya Amani', wala haijawahi kuunga mkono taarifa kama hiyo au kutoa cheti kama hicho."
Cheti 'Fake'
UNESCO imesema jukumu lake ni kustawisha mazungumzo baina ya dini na baina ya tamaduni kote duniani kwa uungaji mkono wa nchi wanachama, washirika na mitandao.

Taarifa hiyo imesema UNESCO inaeneza heshima kwa usawa kwa dini na itikadi zote na daima inajitahidi kuimarisha na kukurubisha watu wote duniani kadiri inavyowezekana.

Taarifa iliyotolewa na mtandao huo Julai 4 ilikuwa hivi:

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na kitengo cha UN cha UNESCO baada ya miezi 6 ya kufanya utafiti kuhusu dini zote za dunia,shirika hilo limetangaza kuwa Uislam ndiyo dini ya amani zaidi duniani .

Utafiti huo ulishirikisha shirikisho la kimataifa la masuala ya amani .

Hayo yalibainika katika mkutano na waandishi wa habari na maafisa wa UNESCO.

Kuhusu ugaidi maafisa hao walisema kuwa Uislam una maana ya amani na hivyo basi ugaidi hauna dini wala kabila .

Waliendelea kuelezea kuwa makundi ya kigaidi kama DAESH yanayotekeleza mashambulizi hadi maeneo matakatifu kama Madina ni thibitisho tosha kuwa hayana uhusiano wowpte na uislam .


Aidha UNESCO itatoa vyeti katika taasisi mbali mbali za kiislamu kama madrassa,vituo vya utafiti vya kiislamu,maduka ya kuuza bidhaa za halal na machinjioni.