Tuesday, 19 July 2016

BREAKING NEWS: SHEIKH KHAMIS SAID KHALFAN AFARIKI DUNIA LEO

Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un (إِنَّا للهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعونَ)  Sura Al-Baqara, aya 156.‎

Sheikh Khamis Said Khalfan amefariki mchana wa saa tisa leo Shawaaal 14, 1437H sawa na 19 July, 2016 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Sheikh Hamis Bin Said
Sheikh said mmoja wa watu wenye elimu kubwa Katika ukanda wa Afrika Mashariki alisifika sana katika elimu na uchamungu.

Sheikh alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu(Blood Pressure) ambapo alipelekwa Hospitali Shree Hindu Mandal na baadae kuhamishiwa Hospital ya Muhimbili.

Sheikh alikwenda Zanzibar kusoma kwa Sheikh Suleiman Alawi na Alhabi Ali Badawi. Pia amesoma kwa Alhabib Omar bin Sumeit huko huko Zanzibar.Alisoma kwa muda wa miaka 21.

Miongoni mwa aliosoma nao huko alikuwa ni Sheikh Abdallah Ayoub kwa miaka minane.

Mwaka 1967 aliruhusiwa kurudi Dar es Salaam. Aliporudi hakuanzisha kusomesha na alianza ziara ya kutembelea Madrasa Kadhaa nchini.

Alienda Madrasa Ya Shamsia (Tamta) na kukaa kwa Sheikh Muhammad Ayoub kwa siku Tisa. Kisha alikwenda Arusha na Lamu. Ziara hiyo ilikuwa ni mwaka 1967 na 1968.

Mwaka 1969 alianzisha Madrasatul Ihyaa iliyopo mtoni kwa Azizi ali jijini Dar es Salaam. Alianza kwa kusomeshea Msikitini.

Mwaka 1970 ndipo alipopata jengo la madrasa na alianzisha Boarding ya Madarsa.

Madrasa hiyo ikaendelea na kupata matawi kadhaa ikiwemo Kilwa Kisiwani na Kilwa Masoko na sehemu kadhaa nchini.

Alizaliwa Kilwa Kisiwani miaka 85 iliyopita. Ameacha mke na watoto kadhaa.




Taarifa zaidi endelea kufuatilia hapa hapa katika Blogu yako ya Ahbaabur Rasuul.

Mwenyezi Mungu amsamehe makosa yake na alifanye kaburi lake kuwa moja ya Mabustani ya peponi.