Shirikisho la wasoma Maulid wa kanda ya ziwa linataraji kufanya mkutano mwishoni mwa mwezi huu huko Kamachumu, Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera.
Mkutano huo unatarajiwa kuanza Tarehe 29/07/2016 hadi tarehe 31/07/2016. Ajenda kubwa katika Mkutano huo ni kuangalia Mustakabali wa wasoma Maulid kanda ya ziwa na nchini kwa ujumla.
Aidha, waumini kutoka taasisi za kiislamu, misikiti na Masheikh kutoka nchini wanaalikwa kuhudhuria mkutano huo, ambapo gharama za malazi na chakula itakuwa juu ya waandaaji ambao ni JUMUIYA YA SHAAFII (R.A).
Mkutano huo ambao ni wa nne kuandaliwa na Jumuiya hiyo wahudhuriaji watajigharamia usafiri wenyewe.
Mkutano wa kwanza ulifanyika nzega mkoani Tabora, wa pili sengerema mkoani mwanza na wa tatu Nyamagana mkoani mwanza.
Taarifa kamili ya mualiko huo soma hapo chini:
TAARIFA YA MWALIKO:-
SHIRIKISHO LA WASOMA MAULID KANDA YA ZIWA:
🌱LINATOA MWALIKO WA
MKUTANO MKUU MUHIMU WA MWAKA 2016 🌱
Mkutano utafanyika tarehe 29/07/2016 hadi tarehe 31/07/2016 eneo la KAMACHUMU,
▶WILAYA YA MULEBA
{Mkoa wa Kagera TZ}
▶SIKU YA KUWASILI ni Ijumaa
tarehe 29/07/2016
Kila taasisi/kundi/ msikiti ilete wawakilishi Wawili kuhudhuria mkutano huu.
👉🏿Mara upatapo mwaliko huu , unaombwa kuthibitisha ushirikiano wako mapema kabla ya tarehe 15/07/2016 kwa kupitia namba hizi:-
👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾
⏩0752179835
Ust Twaha Bakari
⏩0754022219
Ust Ramadhani.H. Chanila
⏩0713350310
Ust Abdurafiu Jaafar Bwanika,
⏩0756551912
Shkh Kamaluddiin Ayoub Salum
Mkutana una ajenda nyingi za muhimu. Kubwa ni mustakabal wa wasoma MAULID.
Wenyeji wa mkutano huu ni :- JUMUIA YA SHAAFII (R.A) IJUMAA na ADHUHURI .
Tunamwomba Allah atukutanishe na tuyatimize mema tuliyoyakusudia kuyajadili
"Nauli kwa washiriki wa mkutano huu watajitegemea, Chakula na malazi ni kwa ni juu ya wandaaji. Inshaa Allah"
Wabillah Tawfiiq
