Watu wa Lut walijiingiza katika vitendo vya kuingiliana wanaume kwa wanaume kulikopelekea kuangamizwa na Mwenyezi Mungu.
Mkasa wa watu hao na kilichowapata rejea Qurani Suratil Araf(7) aya ya 80-84, pale Mwenyezi Mungu aliposema:
وَلُوطًا إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِۦٓ أَتَأْتُونَ ٱلْفَٰحِشَةَ مَا سَبَقَكُم بِهَا مِنْ أَحَدٍ مِّنَ ٱلْعَٰلَمِينَ (٨٠)
إِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ ٱلرِّجَالَ شَهْوَةً مِّن دُونِ ٱلنِّسَآءِ ۚ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ مُّسْرِفُونَ (٨١)
وَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِۦٓ إِلَّآ أَن قَالُوٓا۟ أَخْرِجُوهُم مِّن قَرْيَتِكُمْ ۖ إِنَّهُمْ أُنَاسٌ يَتَطَهَّرُونَ (٨٢)
فَأَنجَيْنَٰهُ وَأَهْلَهُۥٓ إِلَّا ٱمْرَأَتَهُۥ كَانَتْ مِنَ ٱلْغَٰبِرِينَ (٨٣)
وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِم مَّطَرًا ۖ فَٱنظُرْ كَيْفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلْمُجْرِمِينَ (٨٤)
Tafsiri isiyo rasmi
80. Na (tulimpeleka) Luti basi (wakumbushe watu wako) alipowaambia Kaumu yake, je mnafanya jambo chafu ambalo hajakutangulieni yeyote (kwa) jambo chafu hilo katika ulimwengu.
81. Nyinyi mnawaendea wanaume kwa kuwa ndio mnaowatamani badala ya wanawake! Ama ninyi ni watu wafuvaji
82. Na hayakuwa majibu ya kaumu yake isipokuwa kuambizana: "Wafukuzeni katika mji wenu, maana hao ni watu wanaojitakasa (hawataki haya machafu tunayoyafanya. Basi na watoke. Wanakalia nini?)
83. Basi tukamuokoa yeye (Luti) na watu wako isipokuwa mke wake. Alikuwa miongoni mwa waliokuwa nyuma (Wakaangamizwa)
84. Na tukawamiminia mvua kubwa (Ya adhabu). Basi tazama jinsi ulivyokuwa mwisho wa waovu (hao)
Mwisho wa kunukuu
Bila shaka Mufti amelitahadhalisha jambo hilo baada ya kuona kasi kubwa na ushawishi kwa mataifa makubwa kuwalazimisha mataifa mengine kuunga mkono suala la ndoa za jinsia moja.
Hatua ya Mataifa makubwa kutaka kuyalazimisha Mataifa yanayowategemea kwa misaada kuhalalisha ushoga katika nchi zao kama sharti la kupata msaada ni ya hatari zaidi kwani inaupa nguvu ushoga.
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron katika mkutano wa Jumuiya nchi za Madola (common wealth) aliwatangazia rasmi nchi wanachama kuhakikisha suala la Ndoa za jinsia moja linaruhusiwa katika nchi zao kwani ni sehemu ya utekelezaji wa haki za binaadamu na ustaarabu wa wazungu!
Aidha alitahadhalisha kupunguza misaada au kutopewa kabisa kwa nchi ambayo itakataa kutambua haki za mashoga. Tanzania ni mwanachama wa Nchi za Jumuiya ya Madola.
Uganda ambayo imepiga marufuku vitendo vya Ushoga, Usagaji na ndoa za jinsia moja tayari imeanza kuonja joto la kupunguziwa misaada kutoka mataifa wahisani.
Nchini Kenya kama rasmi kwamba mashoga na wasagaji wanaweza kusajili mashirika ya kutetea na kuendeleza haki zao za kibinadamu.
Hii inafuatia uamuzi, wa kihistoria wa mahakama kuu jijini Nairobi, wa majaji watatu ulioiamuru Bodi ya kusimamia Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs) kutambua na kusajili shirika moja ambalo awali mahakama hiyo ilizuia lisajiliwe kwa sababu za kimaadili na kidini.
Mahakama hiyo sasa imeamuru kuwa katiba inaruhusu kutambuliwa na kulindwa kwa haki za 'kila mtu' wakiwemo makundi ya wachache kama vile mashoga na wasagaji.
Serikali inafaa kuendesha masuala yake kwa kuzingatia masharti ya Katiba na haifai kuzingatia misimamo ya dini kunyima kundi fulani la watu uhuru wa kufurahia haki zao,” majaji Isaac Lenaola, Mumbi Ngugi na George Odunga walisema kwenye uamuzi wao walioutoa mwezi April 2015.
Hatua hiyo imekuja baada ya jitihada kubwa za Mashoga kudai kutambuliwa haki zao. Mwaka mmoja kabla ya maamuzi hayo Mashoga walizindua kitabu chao kama hatua mojawapo ya kutaka kukubalika nchini Kenya wiki mbili tu baada ya mwandishi maarufu wa vitabu Bw Binyavanga Wainaina kujitokeza hadharani na kusema kuwa ni shoga.
Kitabu hicho chenye kichwa kisemacho, 'Wasioonekana - Hadithi za Jamii Fiche nchini Kenya', kimeandikwa na aliyekuwa mwanahabari na mwanaharakati wa kutetea haki za mashoga, Bw Kevin Mwachiro.
Kitabu hicho chenye kurasa 114 kinajumuisha mkusanyiko wa hadithi za watu ambao wanadaiwa kupitia hali ngumu baada ya kudhihirika kuwa ni mashoga katika maeneo yote nchini Kenya.
"Wale wote wanaokuza ushoga ni kama wanataka kukomesha kuwepo kwa binadamu,Ushoga si wa kuvumiliwa
katika nchi ya Gambia",aliuambia mkutano wa viongozi wa Dunia mjini New York kwa mujibu wa Gazeti la Huffington Post.
"Hili ni janga na sisi waislamu na waafrika tutapigana kumaliza tabia hii". Aliongeza kwa kusema, "Ulawiti katika namna yoyote ile ni uovu na ni kama kupambana na Mwenyezi Mungu. Hata kama italazimishwa kwa nguvu fulani kuwa ni haki mwanadamu".
Suala la ushoga kwa nchi yetu tayari limeanza kushamiri na kuwa wazi kwa jamii yetu. Sasa mashoga wameanza kujitangaza hadharani.
Tarehe 28 june 2016 sawa na Ramadhani 22, 1437 katika kituo cha Runinga cha Clouds, kipindi cha Take One kinachoongozwa na Mtangazaji Zamaradi Mketema, alifanya mahojiano na Godfrey Majunga maarufu kama Kaoge ambaye alijitangaza kwamba yeye ni shoga.
Aliweka wazi tena bila ya aibu yoyote kwamba anafurahi kuwa katika hali hizo na moja ya 'matarajio' yake siku moja ni kuja kuzaa.
Wengi waliangalia kipindi hicho na kuona kama ni hali ya kawaida. Lakini hili ni ashirio la hatari kwa jamii yetu. Kwamba tunapoelekea ni kubaya zaidi katika swala la ustaarabu na maadili mema.
Jambo kama hilo kwa siku za nyuma lisingewezekana, ama kwa mwanaume kujitangaza yeye ni shoga au hata chombo chochote cha habari kumpa nafasi mtu wa namna hiyo kutangaza upuuzi wake. Ni wazi sasa jamii yetu ipo katika hali mbaya ya kimaadili.
Jingine la kushangaza zaidi katika mahojiano hayo, Shoga huyo alisema kuna NGO moja ipo Hospitali ya Muhimbili ambayo inawatambua kwa kuwapa vilainishi (K-Y Jelly) kwa ajili ya kuzuia michubuko wakati wa tendo, Kondomu pamoja na ushauri nasaha.
Shoga huyo alithibitisha yeye ni mmoja wa wanaohudhuria na kupewa misaada kadhaa katika NGO hiyo.
Kuwepo kwa NGO katika Hospitali ya Serikali ya Taifa ya Muhimbili pia ni kiashiria kibaya kwa kuanza kutambuliwa kwa Mashoga japo kwa njia isiyo rasmi.
Hali ni mbaya kwa jamii yetu, bila shaka hili ndilo lililompelekea Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir kuitahadhalisha Serikali kutoruhusu ushoga na ndoa za
jinsia moja.
Wito wangu kwa masheikh na wanazuoni hili si jambo la Mufti peke yake, ni jambo letu sote tulipigie kelele kwa kulipinga na kuieleimisha jamii ubaya wa jambo hilo na athari zake.
Masheikh wachukue nafasi katika Khutba za swala ya ijumaa, mihadhara mbalimbli, Darsa zao kuitahadhalisha jamii kuwa mbali na mambo ya kishoga na yenye kufanana na hayo.
Aidha wasisitize uboreshwaji wa madrasa kwani huko ndipo kizazi chema kinapotengenezwa. Huko kijana ataandaliwa katika kumuogopa Mwenyezi Mungu kutakapompelekea
kutojihusisha na mambo yasiyo mpendeza Mungu likiwemo hilo la ushoga.
Kasi ya mmomonyoko wa maadili na uhamasishwaji wa ushoga na usagaji duniani dawa na mkombozi wake ni uimarishwaji wa madrasa kwa ajili ya watoto na vijana wa kiislamu.
Madrasa ndio mkombozi wa maadili na akili za watu kwani kwa kupitia madrasa watu watamuogopa mwenyezi Mungu na hawatafanya matendo machafu kama Ushoga na Usagaji.
Kwa sasa dunia inakabiliana na changamoto kubwa ya uhimizwaji wa Ushoga hivyo dawa ya kudhibiti hali hizo ni kuimarisha madrasa na kila mzazi kumpeleka mtoto wake ili
aweze kujengwa katika maadili mema na kujiepusha na maadili yasiyo mazuri.
Madrasa inasimamia malezi bora, inasaidia kujenga khofu na kujenga jamii nzuri. Kwa sasa jamii ina mmomonyoko wa maadili kwa vijana wengi kuiga watu wamagharibi kwa
vijana wa kiume kuvaa hereni, mikufu, kusuka nywele, kuvaa suruali chini ya makalio na wanawake kuvaa mavazi ya kiume.
Hali hiyo ya uigaji inaweza kupelekea vijana ambao hawakupata elimu ya Madrasa kuanza kuiga matendo ya Ushoga kwa kuona ndio ustaarabu na utekelezaji wa haki za
binadamu.
Mwenyezi Mungu katika Qurani ametwambia katika Suratil Nisaa aya ya 110 kwamba:
"Nyinyi mmekuwa umma bora kuliko umma zote, kwa kuwa mnaamrisha yaliyo mema na mnakataza maovu".
Kuamrishana mema na kukatazana mabaya ni sifa za waumini. Katika Qurani tukufu Mwenyezi Mungu ametufundisha kuwa maslahi ya mwanadamu yamo katika kuamrishana mema na katika kukatazana maovu, na kwamba Qaumu nyingi zimeangamizwa kwa sababu ya kutokatazana mabaya na kuamrishana mema.
Twarudia tena tumuunge mkono Mufti katika vita hii dhidi ya ushoga nchini kwetu. Vita hii haina taasisi ni jambo la umma na wala lisiangaliwe nani amesema liangaliwe madhara yake kwa umma.
Wabilah Tawfiq.
