Sunday, 10 July 2016

MHANDISI WA KIMAREKANI ASILIMU SAUDI ARABIA

Mhandisi wa Kimarekani mwenye umri wa miaka 87 ameamua kusilimu baada ya kuishi takribani miaka 55 nchini
Saudi arabia, imeripotiwa katika gazeti la nchi hiyo Alhamis iliyopita.
Mzee Albert katikati aliyevaa shati na suruali
Mhandisi huyo maarufu Albert Hans amekuwa katika nchi ya saudi Arabia akifanya kazi katika visima vya mafuta na kushuhudia tawala za wafalme kadhaa wa nchi hiyo.

Aliamua kusilimu katika mwezi 21 mfungo wa Ramadhani na kuchagua jina la Muhammad huko Bandari ya magharibi ya Red sea.

Mzee Albert ambaye ni mzaliwa wa California, aliingia nchini Saudi Arabia mwaka 1961 na ana wajukuu 24.