Jana jioni mjini Tanga imefanyika zafa kubwa ya chuo kikuu (Mahd) cha kiislamu cha Shamsul Maarif.
Zafa hiyo iliongozwa na Mudir Sheikh Samair Sadiq pamoja na masheikh mbalimbali walishiriki.
Baada ya Zafa usiku kulifanyika Maulid kubwa ya kufunga sherehe za kuadhimisha Elimu zilizoanza jana.
Katika Maulid Masheikh kutoka sehemu mbalimbali walitoa mawaidha.







