Monday, 6 June 2016

BAADHI YA NCHI LEO NI RAMADHANI 1, AFRIKA MASHARIKI KESHO

Baadhi ya Waislamu katika nchi za Kiarabu na maeneo mengine duniani wameanza saumu ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani hii leo. 

Nchi za Yemen, Kuwait, Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu, Jordan, Saudi Arabia na Qatar zimetangaza leo kuwa siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani baada ya kuonekana kwa mwezi. 
Kwingineko, nchi za Kiislamu kama vile Oman, Jamhuri ya Kislamu ya Iran, Morocco na Brunei zimetangaza rasmi kuwa siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni Jumanne Juni 7 baada ya kuthibitika kuwa mwezi haujaandama.  

Aidha Kadhi Mkuu wa Kenya Sheikh Ahmad Muhdhar Jumapili jioni akizingumza mjini Mombasa alithibitisha kuwa mwezi haukuonekana nchini Kenya wala katika maeneo ya Afrika Mashariki na kwa msingi huo akatangaza kuwa Ramadhani itaanza siku ya Jumanne 7 Juni. 

Aidha Kadhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania Sheikh Hamid Masoud Jongo amenukuliwa akitoa tangazo kwa niaba ya Mufti wa Tanzania kuwa  leo Juni 6 2016 ni sawa na 30 Shaaban 1437 Hijria kesho Jumanne itakuwa tarehe Mosi Ramadhani.

Ahbaabur Rasuul inawatakia Ramadhani njema waislamu wote duniani.