Thursday, 2 June 2016

PICHA: UFUNGUZI WA SHEREHE ZA KUITUKUZA ELIMU SHAMSUL MAARIF WAFANYIKA LEO

LEO asubuhi umefanyika uzinduzi wa sherehe za kuitukuza elimu katika Mahd (chuo) Shamsul Maarif iliyoko jijini Tanga katika maeneo ya Duga.

Ufunguzi wa sherehe hizo uliongozwa na Mudir Sheikh Samir Sadiq, Naib Mudir Wake Sheikh Rashid Bakar Al Burhani ambaye aliongoza Dua ya Ufunguzi.
Ufunguzi huo ulihudhuria na watu wengi wakiwemo Sheikh Rajab Kiungiza, sheikh kisuwa Ally na sheikh Simba wote kutoka Arusha.
Bendera ikipandishwa
Aidha kulipandishwa bendera kama ishara ya ufunguzi wa shughuli hiyo ambapo tukio hilo liliambatana na takbira pamoja na Dua.
Mudir Sheikh Samir
Pia palisomwa dua kwa ajili ya kuwarehemu masheikh waliofariki.

Sherehe hizo zitaendelea mpaka siku ya Jumamosi kama kilele na mwisho wa shughuli hizo ambapo hufanyika kila mwaka.

Sherehe hizi ni za kwanza tangu kufariki kwa aliyekuwa Mudir Sheikh Muhammad Bakar Al Burhani. Sheikh Muhammad Bakar alifariki machi 7 mwaka huu sawa na tarehe 26 Mfungo nane 1437 .

Ratiba kamili ya Sherehe hizo waweza kusoma hapo chini.
RATIBA KAMILI

Upandishaji Bendera
Mzee Said Makata rafiki na mwanafunzi wa Sheikh Muhamad Ayoub
Bendera tayari ishapandishwa
Msomaji Qurani 

Wahudhuriaji
Makaribisho
Naib Mudir Sheikh Rashid Bakar Al Burhan
Picha zote kwa Ihsani ya Ustaadh Kambi Mohamed wa Shamsul Maarif,Tanga.