Ratiba hiyo inaonesha ufunguzi wa shughuli utaanza siku ya Alhamisi na kumalizika siku ya Jumamosi ya tarehe 4 juni sawa na Shaaban 28 ndio kilele cha shuhuli hizo.
![]() |
| Mudir Sheikh Samir Sadiq |
Ratiba kamili ni kama ifuatavyo:
👇🏽
Siku: Alkhamisi
Mwezi: Shaaban 26, 1437 Hijr, sawa na Juni 2, 2016
Muda: Saa mbili na nusu
SHUGHULI NA MATUKIO
👇🏽
Utaanza ufunguzi wa shuhuli hizo kwa TAWASULI MAALUM na kuwarehemu Mashekh na Masharifu na Wema waliotangulia na yanayo sindikiza mpaka saa tano asubuhi
✍🏽Baada ya swalah ya ala asri kutakuwa na ziyara ya Sheikh Muhammadi Abibakri (Rahimahullah) na maandamano ya magari pikipik na baskeli kupitia maeneo mbalimbali ya katikati ya mji wa Tanga kwa ajili ya kuonyesha shi'ari ya sherehe hizo za ilmu
✍🏽Maandamano hayo yatakoma wakati wa maghrib katika makao makuu ya Shamsil Maarif Duga.
✍🏽Baada ya swalah ya Isha kutakuwa na Maulidi ya wakinamama
✍🏽Siku ya Ijumaa Shabani mwezi 27 sawa na tarehe 3 Juni saa tano asubuhi mpaka saa tano na nusu khitmah ya Sheikh Muhammad Abibakri Al-Burhaan (Rahimahullah) kuanzia saa tano na nusu mpaka saa sita na nunusu muhadhara sheikh Kisuwa
✍🏽Baada ya swala ya al asri muhadhara ambao kwa kawaida ni Sayyid Abdulqadir Adnan lakini mwaka huu kuna wasiwasi wa kukosekana kama atakosekana nafasi itakuwa ya Sheikh Kiungiza
✍🏽Baada ya isha ni maonyesho ya wanafunzi wa makao makuu ya Shamsil Maarif, wake kwa waume yakisindikizwa na qaswida mpya zilizotungwa na walimu na wanfunzi wa Shamsil Maarif
✍🏽Tarehe 4 juni sawa na Shaaban 28 ndio kilele cha shughuli hizo.
Saa 4 asubuhi mpaka nne na nusu muhadhara kwa kina mama saa tano mpaka sita na nusu muhadhara kwa wote
✍🏽Baada ya alasri Zafa kuanzia Madinah mpaka Duga. baada ya isha maonyesho ya matawi na qaswida mpya mpaka saa 4, saa nne mpaka nne na nusu Samai
✍🏽Zitafuatia khutba za wageni mpaka watapoishia
✍🏽Lengo la shughuli hizi ni kusherehekea na kuadhimisha ILMU nyote mnakaribishwa wake kwa waume
🙏🏽Asanteni sana
