Friday, 10 June 2016

MARUFUKU KUPIGA MUZIKI AU KUCHEZA NCHINI GAMBIA NDANI YA MWEZI WA RAMADHANI

Serikali ya Gambia imetangaza marufuku ya kupiga muziki na kucheza densi kwenye migahawa ya burudani katika mwezi mtukufu wa Ramadhan.
rais Yahya Jammeh
Idara ya polisi nchini humo pia imetoa onyo kali kwa wananchi kutokiuka sheria hiyo iliyozuia muziki na densi mchana na usiku kwa kipindi cha mwezi mzima.

Mkuu wa polisi pia amewataka wananchi kuweka ushirikiano katika suala hilo na kuripoti kesi yoyote ya ukiukaji wa sheria hiyo.

Mnamo mwezi Desemba mwaka 2015, rais Yahya Jammeh alitangaza rasmi Gambia kuwa taifa la Kiislamu.