Thursday, 26 May 2016

USWISI YAWALAZIMISHA WANAFUNZI WA KIISLAMU 'KUWAPA MKONO' WALIMU WA JINSIA TOFAUTI

Mamlaka za kieneo za Uswisi zimepitisha kanuni ya kuwashurutisha wanafunzi Waislamu kuwaamkia kwa mkono walimu wao ambao sio wa jinsia zao, la sivyo watozwe faini ya dola 5,000 za Marekani.

Taarifa ya mamlaka hizo imesema kuwa walimu wana haki ya kumlazimisha mwanafunzi ampe mkono na yeyote atakayekaidi agizo hilo, atatozwa frank 5,000 za Uswisi ambazo ni sawa na dola 5,000 za Marekani.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, maswala ya usawa wa kijinsia na utangamamano miongoni mwa watu wa nchi tofauti, yana uzito kuliko haki ya mwanafunzi kutekeleza itikadi na mafunzo ya dini yake.
Kanuni hiyo imetengua mwongozo uliokuwa umetolewa na shule moja ya manispaa ya Therwil katika wilaya ya Arlesheim nchini humo, wa kukubali ombi la wanafunzi wawili wa Kiislamu wa kiume kutowapa mkono wanafunzi na walimu wa kike, kama wanavyofunzwa na dini yao tukufu ya Kiislamu.

Wanafunzi hao ni watoto wa Imamu wa Msikiti mmoja katika mji wa Basel, raia wa Syria aliyepewa hifadhi na Usiwisi mwaka 2001.