Friday, 27 May 2016

MKUTANO WA KIMATAIFA WA VYOMBO VYA HABARI VYA KIISLAMU WAMALIZIKA

Mkutano wa kimataifa wa vyombo vya habari vya kiislamu umemalizika jana huku mada kuu ikiwa ni kusaidia kukomboa mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.

"Tunapaswakutafuta suluhisho kuhusu masuala ya kibinadamu, kadhia ya Palestina ikiwemo," amesema Fachir katika ufunguzi wa mkutano huo ambapo kaulimbiu yake kuu ni "Vyombo vya Habari vya Kiislamu Vimeungana Kulinda Maslahi ya Uislamu, Hasa Kadhia ya Palestina na Quds."

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Malaysia amepongeza Mkutano wa Kimataifa wa Vyombo vya Habari vya Kiislamu (ICIM) kwa kuweka mbele kadhia ya Palestina ili iweze kuzingatiwa duniani.
Amesema vyombo vya habari vina nafasi muhimu katika mapambano ya kupigania ukombozi Palestina, eneo ambalo limekuwa ikikaliwa kwa mabavu na Israel kwa zaidi ya
miongo sita sasa.

Mkutano huo wa Kimataifa wa Vyombo vya Habari vya Kiislamu umejumuisha washiriki kutoka nchi kadhaa duniani zikiwemo Indonesia, Australia, Iran, Kuwait, Lebanon, Libya, Ufilipino, Malaysia, Nigeria, Singapore, Sudan, Thailand, Tunisia, Uturuki, na Palestina.

Kongamano hilo ambalo limeanza Jumatano limemalizika jana Alhamisi hii katika mji mkuu wa Indonesia, Jakarta.

Mkutano huo wa kimataifa wa vyombo vya habari vya Kiislamu umefadhiliwa na kuandaliwa na serikali ya Indonesia ikiwa ni katiak sera zake za kigeni za kuunga mkono ukombozi wa Palestina.

Mkutano huo ulifunguliwa Jumatano na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia A.M. Fachir