Sherehe kubwa za kuadhimisha mazazi ya mtukufu wa daraja Mtume Muhammad ﷺ zimefanyika Jumamosi hii katika mji wa Hedaru, wilaya ya Same Mkoani Moshi.
Sherehe hizo zilizofanyika katika Msikiti Mkuu wa Hedaru zilianza siku ya Ijumaa kwa maonesho ya elimu kwa wanafunzi.
| Sheikh Shaaban Mbwera |
Aidha Jana jioni ilifanyika zafa kubwa iliyoongozwa na Sheikh Jaafar Sadiq mtoto wa Sheikh Muhammad Albeidh kutoka Malindi Kenya.
| Sheikh Hilal Kipozeo |
Katika kilele cha sherehe hizo siku ya Masheikh mbalimbali walihudhuria wakiongozwa na Mudir wa Shamsul Maarif ya Tanga Sheikh Samir Sadiq
| Sheikh Mahmoud Mustafa |
Wengine waliohudhuria ni Sheikh Said Ali Hassan kutoka Kenya, Sheikh Mahmoud Mustafa Al shiraz kutoka Mombasa Kenya, Sheikh Hilal Kipozeo, Sheikh Shaaban Mbwera, Imamu Msaidi wa Masjid Jumuiya Kisumu Dar es salaam.
| Sheikh Said Ali Hassan |
Wengine ni Sheikh Sheikh Hassan kutoka Mombo, Sheikh wa Wilaya ya Longido, Sheikh Abadallah Jamzuri kutoka Lukozi, Maalim Adam kutoka Bakwata, Kikundi cha Majumuat Jiil salama kutoka Mombasa na wengine wengi.
| Sheikh Jaafar Sadiq |
Msomaji Qurani alikuwa ni Abdallah Rajab na kutoka Dar es Salaam. Aidha Dufu zilipigwa na Madrasatul Shamsul Maarif ya Tanga na Madrsat Fii sabilillah ya Dar es salaam chini Muhammad Muhiya.
| Sheikh Samir Sadiq |
Mwenyeji wa shughuli nzima alikuwa sheikh Yusuf Kidago wa Ahbaabur Rasuul.
MAJUMUATI JIILI SALAMA
MAJUMUATI JIILI SALAMA