Thursday, 14 April 2016

SHIRIKA LA MUUNGANO WA KIISLAMU LAKUTANA LEO ISTANBUL KUJADILI UGAIDI, CHUKI DHIDI YA UISLAMU

Mkutano wa 13 wa Nchi za shirikisho la muungano wa kiislamu unataraji kutafanyika Alhamis leo mjini Istanbul ambapo kutazungumziwa suala la uhusiano baina ya Iran na saudi Arabia, ugaidi na chuki dhidi ya Uislamu inayozidi kuenea.

Wawakilishi kutoka katika mataifa 56 wakiwemo marais 33 na viongozi wa ngazi za juu serikalini watashiriki katika mkutano huo.
Viongozi hao pia wanatarajiwa kuzungumzia hali ya Syria baada ya kumalizika kwa vita nchini humo bila ya kuweka kando suala la wahamaji.

Iyad Emin Medeni, katibu wa shirikisho hilo amefahamisha kuwa mkutano huo wa 13 utakuwa tofauti na mikutano mengine ya hapo awali.

Rais wa Iran Hassan Rohani na mfalme wa Saudi Arabia watashiriki katika mkutano huo kufuatia tofauti zao katika mzozo wa Yemen .