Mwanasiasa huyo aidha anasema kuwa ni sharti Ujerumani izuie ufadhili wa misikiti kutoka Saudi Arabia na Uturuki.
Katibu huyo mkuu wa chama hicho cha CSU ambacho ni mshirika wa chama kinachoongozwa na Kansela wa Ujerumani bi Angela Merkel cha Christian Democratic Union CDU analaumu siasa za kiislamu kwa kuhujumu utangamano baina ya Wajerumani waislamu na wakristo.
Jambo gumu na halikubaliki kuisoma Qurani kwa lugha nyingine, kwa kufanya hivyo kitakachokuwa kinasomwa sio Qurani ni kitu kingine.
