Friday, 15 April 2016

AHUKUMIWA ADHABU YA KIFO KENYA KWA KUMUUA SHEIKH

Mshukiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la CIPK, Sheikh Mohammed Idris amehukumiwa kifo baada ya kupatikana na makosa ya mauwaji.

Akitoa hukumu hiyo, jaji Martin Muya amesema kulingana na ushahidi uliotolewa ni wazi mshukiwa Mohammed Sudi alihusika na mauwaji hayo.

Baada ya kutolewa hukumu hiyo,mke wa mshtakiwa Mwanasha Ramadhan amezirai akiwa nadani ya jengo la mahakama.
Sheikh Muhammad Idrisa
Familia ya mshukiwa imesema inapinga uamuzi wa mahakama na itakata rufaa.

Mnamo Juni 10 mwaka wa 2014, Mohamed Soud, anadaiwa kuhusika katika mauwaji ya marehemu Sheikh Mohamed Idris katika eneo la Likoni.

Mwezi Disemba mwaka jana, Soud, aliwalaumu maafisa wa usalama kwa kumuhusisha na mauwaji hayo,  umiliki wa bunduki na kilipuzi, ikizingatiwa hana ujuzi wa kutumia silaha hizo hata kidogo.