Saturday, 9 April 2016

PICHA: UPANUZI WA ENEO LINALOZUNGUKA AL QA'ABA 'MATAF' LAENDELEA VIZURI

Ukarabati na upanuzi wa eneo linalozunguka Al Qa'aba, 'Mataf' linaendelea vizuri na kutarajiwa kukamilika na kufunguliwa katika kipindi cha mwezi wa Ramadhani amesema afisa mwandamizi.
 Faisal Fuad Wafa, mwenyekiti wa kamati ya ufundi na usimamizi wa upanuzi wa Msikiti wa Makkah, alitoa tangazo katika mkutano wa kamati kwamba pia sehemu zote za ghorofa nazo zitakamilika kabla ya kufanyika kwa ibada ya Hijjah.
 Mradi wa upanuzi wa mataf utaongeza uwezo wake kutoka watu 40,000 mpaka 130,000 kwa saa.