Wednesday, 6 April 2016

UBAGUZI WA DINI: MWANAUME JAHILI AMDHALILISHA MWANAMKE WA KIISLAMU KWA KUVAA NIQABU UINGEREZA

Mwanamke wa kiislamu mwenye umri wa miaka 25 aitwa 'Batman' na mwanaume mmoja jahili kwa kuvalia vazi la usoni la Niqab.

Ahlam Saeed​ alikuwa ameenda katika duka moja huko Shepherd’s Bush ambapo mwanaume huyo alianza kumkejeli mbele ya wanawe wawili.
Mbaguzi wa dini
Mwanamume huyo alizidi kumrushia maneno Ahlam na kumuuliza kwa kejeli sababu ya kuvaa vazi hilo kama 'Batman'.

Mwanamume huyo ameripotiwa kutumia maneno ya ubaguzi aliposema, "Hii ni nchi ya kikristo,tupo katika dunia ya magharibi."

Bi Ahlam alianza maisha yake Uingereza tangu alipokuwa na umri wa miaka 2,na alianza kuvalia Niqab akiwa na miaka 22.

Mwanzoni mbaguzi huyo wa dini hakujua kama Ahlam anajua lugha ya kiingereza na kuendelea kumkejeli.