Monday, 11 April 2016

MSIKITI WA KIHISTORIA CORDOBA,HISPANIA WATAMBULIKA TENA KAMA MSIKITI BAADA YA KUFANYWA KANISA

Baada ya vuta ni kuvute hatimaye msikiti wa kihistoria uliopo katika eneo la Cordoba (قرطبة) umejipatia jina lake halisi na kutambulika kama Msikiti.

Hali ya vuta ni kuvute iliyochukuwa muda wa miaka miwili nchini Uhispania mwishowe msikiti huo umejipatia jina lake halisi.
Msikiti huo ambao unatambulika na UNESCO, kanisa Katoliki lilikuwa limejipa msikiti huo tangu mwaka 2006 kutokana na matatizo ya kisheria.

Msikiti huo katika ramani ulikuwa umetolewa jina lake na kuwekwa jina la kanisa. 
Ramani zote za kitalii neno msikiti lilikuwa limetolewa na baada ya kusainiwa saini zaidi ya 400,000 waislamu wa Hispania kutaka Msikiti huo urudi katika himaya yao na mijadala ya kisiasa kufanyika, msikiti huo umerejeshwa katika uhalisia wake.
Jengo hilo linalowavutia watalii kutoka katika maeneo tofauti huingiza kitita cha pesa milioni 9 kwa Uhispania.​

Msikiti huo uliporwa na wakristo baada ya kuanguka kwa utawala wa Waislamu wa kuitawala Andalus kwa karibu karne nane.
Baada ya mivutano ya muda mrefu wa Msikiti huo kutambulika kama Kanisa badala ya Msikiti sasa umerudishwa na kutambulika asili yake ya mwanzo kama Msikiti.