Sunday, 17 April 2016

MTOTO WA UMRI WA MIAKA 8 ASHIKA NAFASI YA 3 MASHINDANO YA KIMATAIFA KUHIFADHI QURANI MISRI

Musa La Ode(Daudi) Abu Hanafi ameshika nafasi ya tatu katika mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Qurani yanayofahamika kama 'the International Musabaqah Hifzil Quran' (MHQ) yaliyofanyika huko Sharm El Sheikh nchini Misri.

Mussa alishiriki mashindano hayo akiwa amehifadhi juzuu 30 pamoja na washiriki wengine kutoka nchi mbalimbali.
Mussa daudi
Mashindano hayo yalishirikisha vijana 80 kutoka nchi za 60. Baadhi ya nchi zilizoshiriki ni Misri, Sudan, Saudi Arabia, Kuwait, Morocco, Chad, Algeria, Mauritania, Yemen, Bahrain, Nigeria, Malaysia, Brunei Darussalam, Philippines, Thailand, Australia, Ukraine na Indonesia.

Mussa alikuwa ni mshiriki pekee kutoka Indonesia na ndiye aliyekuwa na umri mdogo zaidi kati ya washiriki wote waliokuwepo.

Japo hakushinda nafasi ya kwanza Mussa alipewa heshma ya juu kutokana na umri wake mdogo. Alisoma vizuri Qurani japo kuna matamshi hayakutoka vizuri kutokana umri wake kuwa mdogo sana kuweza kutamka baadhi ya matamko kwa ufasaha zaidi.

Musa anayefahamika kama 'Musa Hafidh' amezaliwa mwaka 2008. Mbali ya kuhifadhi Qurani pia anahifadhi hadith na tayari amehifadhi kitabu cha Imam Nawawiy cha Arubain Nawawiy. Akiwa na umri wa mika 5 na nusu tayri alishahifadhi juzuu 29.
Akiwa na familia yake
Aliwahi kushiriki mashindano ya Jeddah, Saudi arabia na kushika nafasi ya 12 katika washiriki 25 na kuwa ndiye mshiriki mdogo zaidi.


Pia ndiye anayetambulika katika nchi ya Indonesia kama mtu aliyewahi kutokea kuhifadhi Qurani yote akiwa na umri mdogo.