Benki kubwa zaidi ya kiislamu katika Falme za Kiarabu yafahamisha kufungua tawi lake nchini Kenya kabla ya mwisho wa mwaka 2016.
Licha ya mamlaka ya benki za Kenya kutoa leseni mpya kwa benki na kusababisha kufungwa kwa baadhi ya benki muhimu za Kenya,Benki ya kiislamu ya Dubai inasuburi uamuzi wa mwisho kutoka benki kuu ya Kenya ili kuanzisha rasmi utoaji wa huduma zake nchini Kenya.
Benki hiyo ya Dubai itakuwa benki ya tatu ya kiislamu kuendesha huduma zake nchini Kenya.
