Saturday, 16 April 2016

KHITMA YA SHEIKH MUHAMMAD BAKAR, KUTAWADHWA RASMI KWA MUDIR, NAIBU MUDIR KUFANYIKA LEO SHAMSUL MAARIF TANGA

Khitma ya Al marhumu Sheikh Muhammad Bakar Al- burhan inafanyika leo katika Mahdi(chuo kikuu) Shamsul Maarif jijini Tanga leo kuanzia saa nne za asubuhi mpaka adhuhuri mchana.

Aidha sambamba na visomo kwa ajili ya Sheikh Muhammad pia kutatumika nafasi hiyo kutawadhwa rasmi kwa Mudir mpya Sheikh Samir Sadiq pamoja Naib Mudir Sheikh Rashid Bakar,
Mudir Sheikh Samir (kulia) pamoja na Naib wake Sheikh Rashid
Wageni mbalimbali wakiwemo Masheikh kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kuhudhuria shughuli hiyo.

Sheikh Muhammad Bakar aliyekuwa Mudir wa Mahdi(chuo kikuu) Shamsul Maarif ya Tanga alifariki dunia usiku wa Jumatatu ya tarehe 7 mwezi wa Machi mwaka huu jiji Dar es Salaam.

Shekh muhammad Abubakar alizaliwa mwaka 1943 katika kijiji cha Doda wilaya ya mkinga mkoani tanga.

Alianza kusoma masomo ya dini tangu utotoni mwake kwa mwalimu Nabahani  barabara ya sita ngamiani tanga mwanzoni mwa miaka ya hamsini.

Mwaka 1956  alikabidhiwa kwa sheikh Muhammad Ayubu akiwa tayari amekwishakhitimu Qur ani.

Wakati wa uhai wake alisema kwamba alipofika kwa sheikh Muhammad Ayubu alisikilizwa Qurani Suratul Baqara na Sheikh Ayubu aliridhika na usomaji wake kiasi cha siku hiyo hiyo alimkabidhi darsa la watoto wanaojifunza qur ani.

اللهم اغفر له، وارحمه