Sheikh Muhammad alisaliwa swala ya Jeneza wakati wa Adhuhuri na kuzikwa katika Makaburi ya Baqee.
Shekh alizaliwa mwaka 1372H(1952/1953) huko Mji wa Makkah.
Alijifunza kusoma na kuhifadhi Qurani akiwa na umri wa miaka 12 kwa Sheikh Daghistan na Khaleel ibn 'Sheikh Abdulrahman Al-Qari' katika msikiti wa Bin Ladin ulioko Makkah.
Alisoma tafsiri ya Qurani, Sayansi ya Qurani kutoka masheikh kadhaa wakiwemo Sheikh Muhammad Sayyed Tantawi, Sheikh Abdulaziz Mohammed Othman, Sheikh Akram Dhiya Al-Amri, Sheikh Muhammad Al-Amin Al-Shiqiti na Sheikh Abdul Mohsen Al-Abbad.
Ameacha wake wawili na watoto watano.

