Daraja la muda linalozunguka Eneo la Alqa'aba linatarajiwa kuondolewa Mwezi Mei 27 2016.
Kuondolewa kwa Daraja hilo ni kuashiri kufikia mwisho wa kukamilika kwa upanuzi wa ujenzi wa Mataf (eneo linalozunguka Al Qa'aba).
Kwa mujibu wa Kiongozi wa kamati ya kusimamia upanuzi wa Msikiti wa Makkah na Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha
Umm Al-Qura, Bakri bin Matouk Asas amesema jana kwamba 'Mataf' kwa sasa linachukua watu 48,000 kwa saa.
Aidha aliongeza kuwa baada ya kuondolewa Daraja hilo la muda eneo hilo litachukua watu 107,000 kwa saa.
Makadirio eneo hilo likikamilika kabisa ni kuchukua Mahujaji 130,000 kwa saa.
