Uturuki imetoa kitita cha pesa milioni 1,5 sarafu za Marekani kwa ajili ya ujenzi wa msikiti nchini Ghana.
Jengo la msikiti huo unatarajiwa kuwa na uwezo wa kupokea waumini zaidi ya 10,000.
Katika jengo hilo kutakuwa na shule ya kutoa mafunzo kwa maimamu watarajiwa, zahanati, bweni la wanafunzi na ofisi ya idara ya masuala ya kidini nchini Ghana.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na shirika la habari la Anadolu ni kwamba, ujenzi ulianza mwaka 2013 kwa ushirikiano na Profesa Hasan Kamil Yilmaz naibu wa idara ya masuala ya dini Uturuki.
Msikiti huo unatarajiwa kuanza kazi zake mwishoni mwa mwaka 2016.
