Saturday, 12 March 2016

IMAMU WALID ATOA KUMBUKUMBU YA ALIVYOSOMA NA KUMFAHAMU SHEIKH MUHAMMAD BAKAR

Imamu mkuu wa Msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni jijini Dar es Salaam, Sheikh Waleed Alhad Omar ametoa maelezo kuhusu kumfahamu na kusoma kwa Almarhumu Sheikh Muhammad Bakar.

Maelezo hayo ya Imamu Waleed ameyatoa katika Group moja la Whatsaap linalojumuisha Masheikh mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.

Imamu Waleed
Soma kwa ukamilifu maelezo ya Imamu Walid hapo chini:- 

''Assalaam Aleikum Warahmatullah
Imamu waleed (Kushoto) akifurahia jambo na Mudir Sheikh Samir Sadiq. Kulia
ni Doctor Sheikh Mubarak Awes
Nami nijaribu kumueleza Almarhum Sheikh Muhammad Bakar Alburhany rahmatullah alayhi.

Japokuwa ni kazi kubwa na ngumu kutokana na ukweli kwamba bwana huyu alikuwa ni mtu mkubwa sana na haiwezekani mdogo kumuelezea mkubwa bali mkubwa kumuelezea mdogo ni rahisi mno.


Na nitamtaja na kumuelezea rahmatullah alayhi kwa yale niliyoyaona kwake moja kwa moja na kuyasikia kutoka kwake katika muda niliokuwa miongoni mwa wanafunzi wa Shamsiya ktk miaka ya 1980 mpaka 1992.


Au kayasikia toka kwa walioishi nae kabla ya mimi kujiunga na Shamsiyah.

Nimejiunga na Shamsiyah mwaka 1980 nikitokea Riyadha Lamu kenya.


Kabla ya kukutana na Almarhum Sheikh Muhammad Ayoub tulilakiwa na Almarhum Sheikh Muhammad Bakari katika ofisi yake. 


Siwezi kuelezea ukubwa na thamani ya bashasha na ukunjufu wa uso wake uliopambwa na kujawa na ukarimu wa mapokezi yake kwetu, 'subhanallah' Ama kwa hakika wamesema kweli wahenga,

Usimuulizie mtu tabia zake bali (tizama)  paji la uso wake lina ushahidi wa khabari zake. Nilijua hakika huyu ni mtu mwenye
Ukarimu, Uchamungu, Uvumilivu na Upendo kwa watu,
Bali ni mwanachuoni tena ni mwalimu na mlezi.

Alitwambia:
"Mimi huu ni mwaka wa 30 nipo Mzee hapa hapa"

Hamu na hima yake ilikuwa ni 
Kufahamisha kusaidia kubakisha elimu katika jamii.

Siwezi kutaja takhassus yake katika fani ni ipi zaidi ya nyingine bali niseme tu Sheikh Muhammad Bakar alikuwa ni BUKU LA ELIMU.

Na ni msaada mkubwa na marejeo ya elimu  kwa wanafunzi na hata kwa wale waliokuwa waalim zetu kipindi kile.


Chochote alichoulizwa alikijibu kwa ushahidi imma kwa

Qur ani au Hadithi au ubeyti au abyaat za fani husika.

Mwaka 1986 alikuja bwana mmoja toka Lushoto namkumbuka kwa jina moja tu la Ahmed. Alikuja kumuomba Shekh Muhammadd Bakar kwa sheikh Muhammad Ayoub ili ahudhurie Maulid huko Lushoto.


Baada ya kumhoji sana, sheikh Muhammad Ayoub alikubali na kumtoa Ustadh Muhammadd Bakar aende Lushoto maulidini na mimi.

... Njiani nilisoma mengi mnoo...


Tulikaa seat moja mimi yeye na mzee Ahmed. 
Aliniuliza nimehifadhi nini katika swarfa nikamjibu nimemalizia kuhifadhi Nadhmul maqsood.

Alipomaliza akaniambia je katika nahau? Nikamjibu Durratul yatimaTukafanya kama tulivyofanya katika nadhmul maqsood.

Kisha akaniuliza je bayqoon unayo kichwani nikamwambia naam. Pia tukafanya kama tulivyofanya

Akaniuliza je unayo Alfiya ya ibnu maalik nikamwambia hiyo bado sijaianza kuisoma akanambia ni muhimu mno uijue na uihifadhi kisha akaisoma yeye yote beti 1000 mimi nikimsikiliza na kumshangaa.

Akaniambia, 
Waleed vumilia pale Tamta utapata muradi wako. Akasema mimi sasa huu ni mwaka wa 36 bado nipo pale sijatoka nje ya pale bila ya ruhusa ya sheikh kwenda popote na akinitowa kama hivi sijawahi kuzidisha wiki moja.

Zaidi ya mara moja tuliwahi kumsikia Sheikh Muhammad Ayoub akisema "Huyu kaelewa huyu kafahamu"


Sheikh Mohamed Ayoub aliongeza katika manhaj ya dirasaat

Vitabu vifuatavyo; Quratul ayn ktk usululfiqh, Nudh hatunnadhr katika mustwalahul hadeeth, Bullutul uwaami ktk miirathu dhawil arhaam.

Na vitabu vyote hivyo alimkabidhi Almarhuum sheikh Muhammad Bakar atusomeshe. 

Na pia kipindi hicho alikuja Sheikh Abdallah Yusuf Mnyasi Asshiradhiy (kadhi mkuu wa Tanzani) kusoma Hilya ya Balagha kwa sheikh Muhammad Ayoub nae akamkabidhisha kwa Sheikh Muhammad Bakar na pia akawa anahudhuria darasa za vitabu vitatu nilivyovitaja.

Na ananiambia Waleed mwanangu Huyu mwalimu wenu anafahamu kubwa sana na ameelewa vyema ni mwanachuoni wa kujivunia kabisa


Miaka michache nyuma aliandika kitabu cha Swaaiqatul muhrika dhidi ya wale wapingao mambo ya tadawuf na akakisomesha palepale madrasa lakini pia aliandika Almarfaq katika Mantwiq lakini pia aliandika kuhusu miiqat na fanni nyingi kwa lengo la kuungoza umma.


Mwaka 1988 alikuja na changamoto au swali la. باعه Na hilo lilikuja baada ya baadhi ya masheikh na waalimu wa vyuo fulani pale Tanga kusema kuwa Sheikh muhammad Ayoub hakusoma na hajui kitu. 


Sikumbuki kama aliejitokeza kuijibu mpaka muda huu ninayoandika haya.

Almurhum Sheikh Muhmmad Bakar tumemzika jana lakini naamini tumeomkosa mtu ambae ni BUKU KUBWA LA

uchamungu na uvumilivu.
Turathul islami

Ghafarallahu lahu wa askanahu fii fasihi jinaanihi na atunufaishe kwa barka na elimu zake amiin


Sheikh Waleed Alhad Omar

(Dar es Salaam, Tanzania)
10/3/2016   //  30/5/1437