Friday, 11 March 2016

SHEIKH SAMIR SADIQ ATANGAZWA KUWA MUDIR WA SHAMSUL MAARIF YA TANGA

Sheikh Samir Sadiq Hemed leo ametangazwa kuwa Mudir wa Mahdi(chuo kikuu) Shamsul Maarif ya Tanga.

Sheikh Samir ametangazwa kushika nafasi hiyo kutokana na kifo cha aliyekuwa Mudir Sheikh Muhammad Bakar aliyefariki siku ya Jumatatu usiku jijini Dar es Salaam na kuzikwa Tanga Jumatano hii.

Mudir Mpya wa Shamsul Maarif Sheikh Samir Sadiq
Tangazo la kuwa Mudir lilitangazwa na Mushrifu wa Chuo hicho, Mwalimu Rashid Bakar leo alasiri wakati wa Khitma ya Sheikh Muhammad Bakar.

Sheikh Samir Sadiq kwa muda wote alikuwa ndiye Naib Mudir wa Mahdi Shamsul Maarif.
Mushrif Ustaadh Rashid Bakar
Sheikh Samir Sadiq anafahamika kuwa na kiwango kizuri na kikubwa cha elimu ya dini na ni mtu aliyepambika na tabia njema zenye kupigiwa mfano.

Wengi wa wanafunzi na waalimu wa chuo hicho kutoka matawi mbalimbali ya chuo hicho nchini Tanzania wamefurahishwa kwa Sheikh Samir kuwa Mudir wa Shamsul Maarif.

Blogu ya Ahbaabur Rasuul inampongeza na kumtakia taufiq katika majukumu mazito aliyopewa.