Saturday, 5 March 2016

TALAKA ZAONGEZEKA NCHINI UTURUKI

Mji wa Kilis nchini Uturuki umechua nafasi ya kwanza kwa idadi kubwa ya ndoa zinazovunjika baada ya mji wa Izmir kuongoza mnamo mwaka 2015.

Taarifa hiyo ilitolewa na kitengo cha takwimu cha Uturuki cha TUIK katika ripoti yake.
Kwa mujibu wa kitengo hicho ndoa 602,982 zilifungwa na kutolewa talaka 131,830 mwaka 2015.

Asilimia 39,3 za talaka katika miaka mitano ya kwanza ya maisha ya ndoa.

Si tu Uturuki hata nchini Tanzania kumekuwa na talaka nyingi ndani ya ndoa hivyo Masheikh wana changamoto ya kuwaelimisha waumini wao mambo yahusuyo ndoa kabla ya kuingia ili iwe rahisi kumudu changamoto zitakazowakabili.