Monday, 7 March 2016

BREAKING NEWS: SHEIKH MUHAMMAD BAKAR AFARIKI DUNIA, KUZIKWA JUMATANO TANGA

إِنَّا للهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعونَ‎
Mwanazuoni mkubwa ukanda wa Afrika Mashariki Sheikh Muhammad Bakar Al- burhan, Mudir wa Mahdi(chuo kikuu) Shamsul Maarif ya Tanga amefariki dunia leo usiku huu jiji Dar es Salaam.
Taarifa za uhakika kutoka kwa watu wa karibu zimethibitisha. Sheikh Muhammad Bakar aliyepata elimu yake kwa Muhammad Ayoub ameacha wake na watoto kadhaa.

Taarifa zinasema sheikh atazikwa siku ya jumatano mjini Tanga. Wakati wa alasiri. Aidha taarifa zinasema mwili wa marehemu utasafirishwa kesho saa nne asubuhi.

Kwa taarifa zaidi za mazishi endelea kufuatilia blogu yako ya Ahbaabur Rasuul.

Tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu amsamehe makosa yake na amuingize katika pepo ya juu,aamin.