Msikiti wa kihistoria katika eneo la Denya Cyprus Kaskazini umeripotiwa kuchomwa na watu ambao hawakufahamika.
Rais wa Cyprus kaskazini Mustafa Akıncı amelaani vikali shambulizi hilo na kusema kuwa shambulizi hilo sio shambulizi la kawaida bali ni shambulizi la kibaguzi na linalostahili kukemewa.
Hakuna maafa yeyote yaliotokea katika shmbulio hilo wala kusababisha majeruhi.
Tukio hilo limesababisha uharibifu mkubwa kwa mujibu wa kamati simamizi ya msikiti huo.
Rais Mustafa Akıncı amekemea shambulio hilo na kusema kuwa ni kitendo kiovu dhidi ya amani nchini Cyprus.
Rais Akinci ametoa wito kwa viongozi wa Nicos Nicos Anastasiades kufanya kila liwezekanalo ili kuwatia mbaroni waliofanya shambulizi hilo.
